“Msaada Kwanza: Maelezo Mafupi Kuhusu Nyoka” kwa Sanda Ashe
Hatua Muhimu Kusaidia Mtu
Aliyeumwa na Nyoka
Kitakacho fuata ni mbinu au ujuzi rahisi ya huduma ya kwanza kutokana na kuumwa na nyoka ya sumu. Soma maagizo kamili kwa makini. Ikiwa wewe au mtu yeyote karibu nawe ameumwa na nyoka mwenye sumu kali basi unaweza kupunguza maumivu hayo ama madhara yake kwa kuwa mwangalifu kuhutibu kwa njia unaofaa kwa maagizo bora.
Ukiwa Shambani au Njiani:
Ikiwa yule nyoka aliyekuuma utamuua, basi ni vyema pia umuweke mahali pazuri hadi kwa daktari. Lakini kama nyoka hukumuona wakati wa ajali, wewe usipoteze wakati ukimtafuta. Ni vizuri utafute nija ya kumsuadia yule aliye pata ajali kwa njia ya haraka iwezekanavyo.
Wakati wa ajali yoyote kama hasara ya kuumwa na nyoka ni vizuri yule msaidizi au muhuduma yeyote awe mtulivu na mwenye kutia moyo kwa aliyepata ajali hiyo. Si vizuri kuruhusu wapita njia au watu wengine wa jamii wenye kubabaika wanapona ajali kama hii, kukaa karibu na mgonjwa. Mara nyingi watu huzidiwa na hali mbaya na mara nyengine hufakwa sababu ya kutiwa hofu na wasiwasi. Wakati wa ajali kama hii, weweyakupasa uwe mtu wa kujipa moyo. Usiruhusu watu wakutie hofu hata nyoka awe mkubwa kiasi gani.
Mtu aliye pata hasara kama hii anapaswa kusaidiwa kwa kuondoa vitu vyovyote kama saa ya mkono, bangili, ama hata nguo ambayo inamshika sana. Wakati ukifanya harakati za kumpeleka aliyeumwa na nyokakwa daktari, hakikisha ule mguu au mkono ule ulio umwa umezuiliwa na kama vile kipande cha nguo. Kinyume na desturi, usimfunge kitu chochote iwe ni mkono au mguu ulioumwa. Unapofunga mahali palipo umwa unazuia damu kuzunguka mwilini. Hivyo basi athari za ile sumu husababisha uharibifu mkubwa katika mguu au mkono ule. Mara nyingi damu inapokosa kuzunguka vizuri, mguu hufura zaidi.
Hakikisha kwamba wakati munapoenda kwa daktari, unajaribu kujua habari muhimu kuhusu aina ya yule nyoka. Hivyo utasaidia kutoa habari muhimu kwa haraka ikiwa yule mgonjwa atakuwa hali mbaya ya kushindwa kupeana maelezo mwenyewe.
Ni vizuri kuhakikisha ya kwamba unafahamu ni wapi unaweza kupata dawa ya kipekee ya aina ya ‘Antivenom’. Jua ya kwamba dawa hii ya nyoka iliyo ya kipekee, ni bei ghali na kwa hivyo si rahisi kupatikana katika hospitali ndogo ama maduka yote ya dawa. Ushauri wangu ni kwamba watu wa kijiji waweza kujiunga na kununua dawa hizi na kuweka mahali palipo na ‘refrigerator’ kwa manufaa ya watu wa kijiji chote.
Kuwa makini wakati unasafiri hospitali. Ikiwa uchungu unazidi unaweza kutumia dawa aina ya Panadol. Kumbuka ya kwamba damu inapokuwa haizunguki kwa mwendo wa sawa mwilini yawezakuwa sababu ya kumfanya mgonjwa azirai. Wakati amezirai, wewe unaweza kusaidia kwa kuinua miguu yake hadi hali ya usalama imurudie huyo mgonjwa.
Mara nyingine nyoka anaweza hata kusababisha kidonda kikubwa. Usipokuwa na tahadhari basi mahali pale paweza kusababisha mguu ukatwe au hata kifo. Vidunda vya aina hii visipochunguzwa na daktari na kutunzwa vizuri, mwishowe huwa donda ndugu na vyaweza kupozesha mguu.
Jinsi ya Kutibu Aliyetemewa Sumu kwa Macho na Nyoka:
Ikiwa yule nyoka amekutemea mate kwa macho, basi osha macho yako kwa maji mengi. Lakini, mahali hakuna hata maji, unaweza kutumia mkojo safi kuosha macho pekee. Kila sehemu ya mwili iliyomwagikiwa na sumu lazima ioshwe vizuri.
Lile jicho liloathiriwa huenda likawasha kwa muda na hata pia kutokwa namachozi huku pia mate yakijaa mdomoni.
Pangusa kutumia kitambaa safi kuelekea nje ya jicho, ili usiruhusu sumu kurudi ndani ya jicho.
Kumbuka ya kwamba sio nyoka wote wana sumu.
Hakikisha ya kwamba mgonjwa anapata chakula kilicho na maji mengi.
Ikiwa mgonjwa anashida ya kupata mkojo, tafadhali umpeleke kwa daktari.
Wakati huu anopoendelea kupata nafuu mgonjwa anaweza huhisi uchovu ama hata pia kuzirai. Ni vizuri awe na mahali pazuri pa kujituliza.
Kama mahali palipoumwa kunatoka damu, kidonda hicho lazima kiaguliwe kwa hali ya usafi, kulingana na maagizo ya daktari hadi mgonjwa apone. Vidonda kama hivyo vyaweza kuleta madhara makubwa kiasi cha kumfanya mtu kuwa kiwete au kukatwa mkono. Kwa hivyo nivizuri kujifunza kujua jinsi ya kuepuka janga kama hili.
Hatua Rahisi za Kuishi kwa Usalma Katika Maeneo ya Nyoka Wengi:
Kumbuka kwamba nyoka wote ni hatari. Hata hivyo, mara hyingi huishi kwa kuua wanyama wadogo, kama vile panya, hivyo basi kuzuia kueneza kwa magonjwa mengineyo. Wao pia hula aina ya denge amabo pia wakiwa wengi mno huleta uharibifu wa mimea shambani. Ninakushauri kwamba, ujaribu uwezavyo kuona ya kwamba si kila nyoka unayemuona njiani astahili kuuliwa. Ni vizuri kuwatunza kiasi kama raslimali asili ya dunia hii. Lakini tujihadhari sana kwani aina chache za nyoka wanayo sumu kali inayoweza kuhatarisha maisha yako, kwa hivyo ni vizuri tuzingatiye maelezo machache yafuatayo.
Ukiwa kwa boma lako, jaribu sana kujenga kibanda cha mifugo, sana kibanda cha kuku na bata au hata sungura.
Jaaribu iwezekanavyo kuweka chakula mahali ambapo panya hawawezi kufanya makao kwa sababu nyoka ataingia ndani kwa kutaka kuwala.
Jaribu kuhakikisha mahali pa kulala kumeinuliwa juu, huku ikiwezekana, pia utumie ‘neti wa umbu.’
Safisha manyasi marefu kando ya nyumba yako. Pia si vizuri kuweka mrundo mkubwa wa kuni karibu na nyumba ya kulala, kwani hivyo ni kuwajengea mahali pa kulala wale nyoka.
Pia si vyema kuwa na miti ya kivuli ikilalia nyumba kwani nyoka pia hupenda sehemu za utulivu kama hizo.
Kuku na wanyama wengine wa nyumbani hutoa mlio fulani wa kutahadharisha kitu kisicho cha kawaida. Kwa hivyo chunguza uonapo mifugo wako wakionyesha kitendo lisicho cha kawaida.
Usiweke mkono wako ndani ya mashimo, bila kujua ni wanyama aina gani inaoishi hapo ndani.
Kuwa makini wakati unaposafisha msitu shambani mwako. La muhimu ni kwamba iwapo utaumwa na nyoka wakati wowote jaribu kufika kwa daktari haraka iwezehanavyo.
Utangulizi. Kwanza kabisa, ningependa kutoa shukran zangu kwa wale wote waliosaidia,waliodhamini, waliotoa hotuba na hata wale wote waliohudhuria washa ya pili ya Kutoa Huduma ya Kwanza kwa walio umwa na Nyoka, kule hoteli ya Hemingways, Watamu, Kenya.
Hii ni ile orodha Kamili ya waliohotubia:
Bw. James Ashe, Bio-Ken Snake Farm, PO Box 3, Watamu
Dk. Harry Mwimali, Veterinary Clinic, PO Box 99, Malindi
Bi. Damaris Rotich, Curator of Herpetology, National Museums of Kenya, PO Box 40658, Nairobi
Dk. James Southern, South African Vaccine Producers (pty) Ltd, Reintfontein, PO Box 28999, Sandringham 2131, South Africa
Prof. David Theakston, Liverpool School of Tropical Medicine, Pembroke Place, Liverpool L3 5QA, England
Prof. David Warrell, John Radcliffe Hospital, Headington, Oxford OX3 9DU, England Ningependa kumshukuru Prof. Warrel na Bw. Ashe kwa usaidizi wao katika maelezo ya kijitabu hiki.
